NJIA BORA ZA UHIFADHIJI WA CHAKULA
Chakula kinaweza
kuhifadhia au kutunzwa kwa matumizi ya baadae kwa kupitia njia mbalimbali, watu
wa zamani hawakuwa na technologia kama tuliyonayo wakati wa sasa hivyo walikuwa
wakitumia njia mbalimbali kuhifadhi chakula kwa ajili ya matumizi ya
baadaye,njia za kuhifadhi chakula zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni
njia za kisasa na za asili
NJIA ZA ASILI
Hizi ni njia ambazo
hutumia , vitu vya asili katika kufanya chakula kisiweze kuharibika,njia hizi
ni kama zifuatavyo
CHUMVI NA SUKARI
Hapa ni pale ambapo
chumvi, sukari au vinega huwekwa au kupakwa katika vyakula vya nyama ambapo husababisha chakula
hicho kukauka kabisa na hivyo bacteria hushindwa kukaa mahali hapo na
kukishambulia chakula hicho, mfano wa vyakula hivyo ni kama samaki, nyama
nakadhalika, lakini pia njia hii husaidia kuongeza ladha nzuri kwenye chakula
KUKAUSHA JUANI
Njia hii hutumika kutunzia vyakula kama mahindi, mchelo,ndizi,maharage ,samaki ,mihogo, mboga za majani n.k
Njia hii ya kukausha na jua ni njia bora ambapo chakula huachwa juani kwa mda mrefu mpaka pale kitakapokauka kabisa na maji yote kuondoka na kukiacha chakula hicho kuwa kikavu kabisa hii hufanya bacteria ambao huaribu chakula kushindwa kabisa kukaa kwenye chakula hicho, vyakula kama ndizi na mihogo hukatwa katika vipande vidogo vidogo ili kuviwezesha kukauka haraka
MOSHI
Moshi pia hutumika katika
kukaushia chakula ambapo chakula huwekwa juu ya kichanja na kwa chini moto
huweshwa lakini kinachotakiwa ni moshi tu na sio moto, moshi wezeza kukausha
chakula hicho na kuondo kiwango cha maji kabisha na kusababisha bacteria
kushindwa kuishi humo, vyakula kama nyama,samaki na mbagomboga vinaweza
kukaushwa kwa njia hii
KUPIKA
Kupika kunahusisha
kuchemsha,kukaanga n.k njia hii ya kukipika chakula husaidia kuuwa bacteria
ambao huwepo ndani chakula hizo na kukiacha kikiwa salama , vyakula kama viazi,
ndizi , mihongo, samaki, nyama n.k vinaweza kuchemshwa kwanza halafu ndio
vikakaushwa
UCHACHUSHAJI
Lakini pia chakula
kinaweza kuchachushwa kwa mfano vyakula vya kabohydreti kama sukari huweza
kubadilishwa na kuwa alcohol au maziwa freshi kubadilishwa na kuwa
mtindi,vyakula kama matango na maembe huweza kuchanganywa na chumvi, na baada
ya mtu lactic acid huzalishwa kukifanya chakula kuwa na ladha nzuri na
kukiwezesha kukaa mda mrefu
NJIA ZA KISASA
KUTUMIA
FRIJI
Hii ni njia ya kutunza
chakula katika joto la chini sana ya sentigredi kutunza chakula katika joto la
chini sana ya sentigredi 4 ambapo hufanya shughuli za bacteria kupungua
na hivyo chakula huweza kudumu kwa mda mrefu bila ya kuharibika
Hapa ni pale ambapo
chakula huweza kugandishwa kabisa chini ya nyuzi joto -10 ambapo huzuia kabisha shughuli za
bacteria wanaoharibu chakula kufanyika, vyakula mfano samaki, nyama vinaweza
kugandishwa kabisa kwenye freezer na kufanya chakula kudumu kwa muda mrefu.
KUCHEMSHA
(PASTEURIZATION)
Hii ni njia ambayo
ilipewa jina na LOUIS PASTEUR ambapo chakula
huchemshwa katika nyuzi joto za juu sana illi kuuwa bacteria ambao huleta
uharibifu wa chakula, lakini pia njia hii husaidia kuongeza ladha kwenye
chakula, vyakula ambavyo vinaweza kuchemshwa ni kama maziwa pamoja na juice za
matunda
UYEYUSHAJI
AU ULAINISHAJI WA VYAKULA
Hii ni njia ambayo
hutumika kufanya vyakula kuwa katika mfumo wa kimiminika kwa mfano matunda
husagwa na kuwa juice na kisha kuchemshwa
na kuwekwa kwenye makopo ya kuhifadhiwa
KUTUMIA
KEMIKALI
Pia chakula kinaweza
kuhifadhiwa kwa kutumia kemikali mbalimbali kama sodiam benzoate, sodiam
chloride na vinegar huwekwa kwenye chakula kwa ajili ya kuzuia bacteria kufanya
shughuli zao, hivyo husaidia chakula kukaa mda mrefu bila kuharibika
KUTUMIA
MIONZI
Chakula kinaweza
kupitishwa kwenye mionzi ambayo husaidia kuuwa bacteria waliopo kwenye chakula
hicho na kukiacha kikiwa salama, vyakula hivyo vikiwemo vitunguu, viazi, maharage n.k
SOMA ZAIDI KUHUSU

