mlo kamili

 MLO KAMILI

  Kula mlo kamili husaidia kukuza afya njema, lishe bora hutokana na mlo wenye vyakula kutoka kwenye makundi yote ya vyakula kwa uwiano sahihi, mlo kamili husaidia mtu kubaki na afya njema. Lakini pia mlo kamili humsaidia mtu kukua na kuendele pia husaidia kudumisha uzito bora wa mwili, zaidi ya hayo hupunguza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya muda mrefu kama saratani, kisukari, uzito uliokithiri, shinikizo la damu na magonjwa mengine ya kutishia maisha.

Kula mlo kamili kunamaanisha kula aina mbalimbali za vyakula kwa uwiano unaofaa, kula vyakula vyenye vitamin na madini mbalimbali lakini pia matunda au kunywa juisi iliyojaa vitamini na virutubisho kunaweza kusaidia kufikia na kudumisha uzito wa mwili.

Jinsi ya kutengeneza lishe yenye afya

Kula mboga na matunda zaidi

Kula mbogamboga za majani pamoja na matunda, lazima ulenge aina tofauti za matunda kama mananasi, machungwa, maembe,

  Kula protini

Kuna faida nyingi za kujumuisha protini kwenye milo yako kwani husaidia mwili kuwa na afya bora na kupambana na magonjwa ya aina mbalimbali, protini ni pamoja na nyama, samaki, kuku, maharage, na karanga n.k

kabohaidreti

kabohaidreti ni chanzo kizuri cha nishati, ni muhimu kula kabohaidreti ya kutosha kwani husaidia mwili kupata nishati zaidi baadhi ya vyanzo vya wanga ni pamoja na mchele, nafaka nzima na maharagwe.

Unaweza kuchagua aina ya vyakula vya wanga kwenye mlo wako kama vile wali wa kahawia, pasta ya ngano nzima, vyakula vyenye nyuzinyuzi kama mihogo n.k

Tumia mafuta ya mimea yenye afya

Jenga tabia ya kutumia mafuta ya kiafya yatokanayo na mbogamboga vyanzo vingine vya mafuta ni pamoja na olive oil, canola, soya, mahindi, alizeti, karanga na mengine, epuka kutumia mafuta mengi kwani yanaweza kusababisha kuongezeka uzito au kumfanya mtu kunenepa. hatimaye inaweza kusababisha uzito uliokithiri

Maziwa na vyakula vya maziwa

Vyakula vya maziwa na maziwa ni bora zaidi kwa utunzaji wa afya kwa mfano mtindi na jibini ni vyanzo vizuri vya mafuta na protini, vina calcium, ambayo husaidia kuweka mifupa yako yenye afya.

  KWA NINI MLO KAMILI NI MUHIMU SANA?

hudumisha afya

Kuwa na afya bora ni muhimu sana, kula chakula bila kuzingatia virutubisho kunaweza kusababisha baadhi ya matatizo ya kiafya kwa mfano kula mafuta mengi kunaweza kusababisha unene na kisha kupata magonjwa ya moyo kama presha na mshtuko wa moyo, magonjwa mengine yanaweza kujitokeza kutokana na ulaji mbaya. kwa mfano kwashiorkor ambapo mtoto anakuwa na tabia ya kula chakula kingi, marasmus na kadhalika

huimarisha mifupa.

Lishe bora ni pamoja na vyakula mbalimbali ambavyo vina baadhi ya madini na virutubishi ambavyo vina mchango mkubwa katika kuimarisha mifupa kwa mfano madini ya kalsiamu ndiyo bora zaidi kwa kujenga mifupa imara.

Kuboresha kinga

Kinga ya mwili inaweza kuboreshwa kwa urahisi na mlo tunaokula ndiyo maana ni muhimu kula kila aina ya virutubishi vinavyopatikana katika vyakula vya aina tofauti tofauti kama , matunda, vyakula vyenye nyuzinyuzi, mbogamboga, wali, mihogo na kadhalika. .

Kutoa nishati ya mwili

Mtu anapojishughulisha na kazi ngumu anaweza kuhitaji nguvu nyingi na kitu kizuri kuna vyakula ambavyo ni bora pale linapokuja suala la kuupa mwili nguvu, vyakula hivyo ni pamoja na mihogo, wali, viazi, mahindi n.k

  Ni magonjwa gani ambayo yanaweza kusababishwa na ukosefu wa lishe bora?

Kuna athari nyingi za kutotumia lishe bora, magonjwa mengi husababishwa na ulaji mbaya ,magonjwa haya yanaweza kujumuisha.

Unene kupita kiasi

Watu wanaokula bila kuzingatia maudhui ya kile wanachokula wako hatarini kupata matatizo ya kiafya, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi kama nyama, soseji, siagi na kadhalika huweza kusababisha unene uliokithiri lakini pia ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi  huweza kusababisha tatizo la kiafya kwa sababu sukari iliyozidi mwilini hubadilishwa kuwa mafuta na kisha kuhifadhiwa mwilini kwa matumizi ya baadaye, mrundikano wa mafuta haya unaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito na hatimaye unene.

Matatizo ya moyo

Watu wenye unene pia wanaweza kukumbana na tatizo lingine la kiafya kama vile matatizo ya moyo, moyo utashindwa kufanya kazi yake ya kusukuma damu kutokana na mrundikano wa mafuta mengi kwenye misuli hii inaweza kusababisha mshtuko wa moyo au shinikizo la damu.

Saratani

Saratani pia inaweza kukuzwa kupitia tabia mbaya ya ulaji, watu wanaovuta sigara kupita kiasi, unywaji pombe, kafeini, tumbaku wapo katika hatari ya kupata saratani ni muhimu tukaondokana na vyakula ambavyo vinaweza kuhatarisha afya zetu.

 

Chakula chenye afya kinajumuisha nini?

mlo wenye afya unajumuisha matunda na mboga mboga nyingi n.k  Ili kuwa mtu mwenye afya, ni muhimu kula vyakula vyenye mafuta kidogo, sukari na chumvi, lakini kuwa na kiasi cha wastani cha vyakula vyenye protini, wanga, vitamini, madini na nyuzinyuzi, ni muhimu pia kunywa maji ya kutosha na kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara

Zingatia yafuatayo ili kuwa na afya njema

Kuchukua kiasi kilichopendekezwa cha protini mafuta, sukari na chumvi, Chukua kiasi kilichopendekezwa cha matunda na mboga katika mlo;

Kula vyakula mbalimbali vikiwemo nafaka, matunda, mbogamboga na vyakula vyenye nyuzinyuzi ili kuupa mwili nguvu na lishe inayotakiwa.

Fanya mazoezi ya viungo au mazoezi kila siku kwa dakika 30 hadi 40 inaweza kusaidia kuboresha kinga ya mwili na kuimarisha mwili

Badilisha lishe ya nyama nyekundu na samaki, kuku au nyama konda

Tumia maziwa yenye mafuta kidogo na vyakula vyenye chumvi kidogo

Punguza utumiaji wa vinywaji vya sukari na pipi na Epuka vyakula vilivyosindikwa na kuokwa vya kila aina

NENO LA MWISHO

Matatizo mengi yanaweza kuepukika kwa kula mlo kamili, tatizo kama unene, kwashiorkor, marasmus, rickets na kadhalika, mlo kamili unachangia sana kujenga na kuimarisha kinga ya mwili, wazee, wagonjwa, vijana, watoto, akina mama wanaonyonyesha hawa ndio kundi muhimu zaidi la watu wanaohitaji uangalifu mkubwa linapokuja suala la lishe yao.

SOMA ZAIDI KUHUSU

tabia hatarishi

Jinsi ya kuwa imara kiakili na kimwili

Mambo muhimu kuyajua unapokuwa mtu mzima

Msongo wa mawazo

Afya ya akili

Jinsi ya kupunguza uzito

Namna ya kufanikiwa

Post a Comment

Previous Post Next Post