tabia hatarishi

 TABIA HATARISHI

Tabia hatarishi hizi ni tabia ambazo huweza kuweka maisha ya mtu kwenye hatari ya kuathirika kiafya lakini pia huweza kuathiri hali ya kimwili na kiakili ya mtu Fulani, wapo watu mbalimbali ambao wameathirika na tabia ambazo sio nzuri na zimeendelea kuwatesa katika maisha yao, hapa nitaelezea baadhi ya tabia ambazo ni hatarishi katika jamii na katika maisha ya mtu binafsi

UVUTAJI WA BANGI NA KUTUMIA MADAWA

Wapo vijana ambao hujihusisha na tabia kama hizi ambazo ni mbaya za uvutaji wa bangi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya, ambayo huweza kuleta madhara ya kiafya, pamoja na kusababisha  mmong’onyoka wa maadili, uvutaji wa bangi pia huweza kuleta madhara mengi kiakili  kwa mfano mtu anaweza kurukwa na akili kwa sababu ya kuvuta bangi kupita kiasi

Pia utumiaji wa madawa ya kulevya husababisha upotevu wa nguvu kazi kwa vijana, vijana wanaotumia madawa ya kulevya hawawezi tena kufanya kazi ngumu na hata hamu ya kula hupungua kadiri siku zinavyozidi kwenda

UKAHABA

Ukahaba ni tabia ambayo huweka maisha ya wahusika katika hatari za kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya zinaa na ukizingatia yapo baadhi ya magonjwa ambayo hayana tiba kwa mfano ugonjwa wa UKIMWI n.k vijana wengi hujihusisha katika tabia hizi za ukahaba na hivyo kupelekea kukatisha ndoto zao za kimaisha ikiwemo kupata elimu n.k

MAPENZI YASIYO SALAMA

Kitendo cha kujihusisha na mahusiano na mpenzi Zaidi ya mmoja ni hatarishi sana lakini pia kushiriki katika kufanya mapenzi bila hata ya kutumia kinga huweza kuweka afya ya mtu katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa kama UKIMWI, KISONONO na KASWENDE

UENDESHAJI CHOMBO CHA MOTO VIBAYA

Kuendesha gari,pikipiki, bajaji nk vibaya kunaweza kupelekea ajali kutokea na mwisho kusababisha vifo,lakini pia hupaswi kuendesha gari au pikipiki ukiwa umelewa na umetumia madawa yanayoweza kuleta kizunguzungu, unapoendesha gari unapaswa kuvaa mkanda na kuchukua tahadhari zote zinazotakiwa

ULAJI MMBAYA

Ulaji mmbaya unaweza kuweka afya ya mwili katika hatari ya kupata matatizo ya kiafya kwa mfano mtoto anapokula kupitiliza anaweza akapata kiribatumbo, mtu ni lazima ale mlo uliokamili ambao unamchanganyiko wa vitamini, madini n.k

Lakini pia vyakula vinavyoongeza nguvu kama mihogo,wali,ugali,kande n.k humsaidia mtu kupata nguvu ya kufanya kazi ngumu

Mtu ni lazima kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi kama keki,chokoleti nk  sukari inapokua nyingi katika mwili huweza kubadilishwa na kuwa mafuta hivyo huifadhiwa ndani ya mwili kwa matumizi ya baadae hii huweza kupelekea kuongezeka uzito au unene baada ya mda Fulani.

KUJIDHURU

Wapo baadhi ya watu ambao wanapojisikia kuvunjika moyo au kuchanganyikiwa huamua kujidhuru aidha kwa kujiua au kujikatakata na viwembe ambayo huleta madhara makubwa katika mwili wa mhusika n ahata kifo

UUZAJI MBAYA WA BIDHAA AU UTEKAJI

Zipo bidhaa ambazo zinauzwa kimagendo lakini pia zipo bidhaa ambazo ni hatarishi na hazijathibitishwa na mamlaka husika kuweza kutumika katika jamii Fulani bidhaa za namna hii huweza kuleta madhara makubwa katika jamii na hata kusababisha kifo  kwa mhusika, uuzaji wa bidhaa hizi ni tabia mojawapo ambayo ni hatarishi na inaweza kumsababishia mtu kifungo cha mda mrefu gerezani lakini pia wapo watu wengi ambao wamepotea katika mazingira ya kutatanisha hii inatokana na kutekwa nyara na pengine hata kunyofolewa viungo vyao kwa ajili ya pesa kujihusisha na tabia au makundi ya watu wa namna hii kunaweza kupelekea kifungo, kifo au hata kufanyiwa kitu kibaya endapo mtuhumiwa akikamatwa

UCHEZAJI WA KAMARI

Kamari pia ni mojawapo ya tabia ambazo ni hatarishi sana, watu wanaocheza Kamari pia hujihusisha sana na tabia za wizi, uporaji, ukabaji na hata kuteka nyara, ni vyema kuwa makini sana na watu wenye tabia za namna hii lakini pia kusaidia kuwarekebisha kama itawezekana

BIASHARA HATARI ZA MITANDAONI

Mtu pia anaweza akawa anajihusisha na tabia hatarishi za mitandaoni  ikiwemo kufanya udukuzi kwenye account za watu kwa ajili ya kuiba fedha au taarifa Fulani, lakini pia biashara haramu za uuzaji wa silaha,madawa ya kulevya n.k zinaweza pia kufanyika online

WAZO LA MWISHO

Ni vyema kuzitambua tabia hatarishi na kujua namna ya kuziepuka, baadhi ya tabia huweza kuleta maafa,vifo, kuibiwa n.k ,zipo tabia nyingine nyingi ikiwepo unywaji wa pombe, ubakaji, utapeli n.k

SOMA ZAIDI KUHUSU

Kwanini maisha ni magumu

Jifunze kuhusu ndoto

Afyaya akili

Jinsi ya kufanikiwa kiuchumi

Tabia za mtu aliyefanikiwa

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post