JINSI YA KUWA IMARA KIMWILI NA KIAKILI
Msingi wa kuwa na furaha
ni kuwa na afya njema ya akili pamoja na ya mwili,kujiweka imara kimwili na
kiakili kuna faida nyingi sana ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kukusaidia
kupunguza uzito kama una uzito uliokithiri lakini huupa ubongo nguvu ya kufanya
kazi zake kwa ufanishi,
Mtu anapokuwa imara kiakili na kimwili huweza kufanya maamuzi kwa ufanisi, lakini pia humpa mtu nguvu ya kufanya kazi zake kwa bidi, pamoja na hayo uwezo wa kuwa imara kimwili na kiakili unapaswa uzingatie mambo yafuatayo
KUFANYA
MAZOEZI
Ni lazima ujiwekee ratiba
ya kufanya mazoezi kila siku au angalau siku 3 ndani ya wiki moja, mazoezi
husaidia kupunguza kiwango cha mafuta katika mwili na hivyo humwezesha mtu
kupungua uzito na ndo maana kwa wale ambao uzito wao umezidi wanashauriwa
kufanya mazoezi mara kwa mara,lakini pia mazoezi huimarisha kinga ya mwili na
kufanya akili kuwa imara, mazoezi mazuri ni yale yanayohusiana na kuongeza
msukumo wa damu katika mwili, kunyoosha viungo, kwa mfano mazoezi kama ya
kukimbia, kuruka Kamba n.k
EPUKANA NA
MSONGO WA MAWAZO
Katika shughuli
mbalimbali tunazozifanya huwa tunakutana na changamoto mbalimbali ambazo
zinaweza kutusababishia kuwa na msongo wa mawazo, kutokana na hali hiyo ni
muhimu kujua namna utakavyoweze kukabiliana na msongo wa mawazo,msongo wa
mawazo unaweza ukakusababishia kuwa na hofu, maumivu ya kichwa,kukosa uelekeo
katika malengo yako, soma Zaidi namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo hapa
KULA MLO
KAMILI
Mlo kamili ni muhimu kwa
afya yako hivyo ni muhimu mtu apate mlo kamili ambao utakuwa na virutubisho vya
aina mbalimbali pamoja na madini, vyakula kama ugali,wali,viazi, mihogo,
maharage,mboga za majani, matunda n.k hivi vyakula huweza kuimarisha kinga ya
mwili na kumfanya mtu awe imara kimwili na kiakili lakini pia mtu huweza
kuepukana na magonjwa mbalimbali ikiwemo presha, mshtuko wa moyo,uzito
uliokithiri n.k
PATA
USINGIZI WA KUTOSHA
Kukosa usingizi wa
kutosha kunaweza kuathiri afya ya mwili pamoja na ya akili hivyo inashauriwa
mtu aweze kulala angalau kwa masaa saba au nane hii huufanya mwili pamoja na
akili kupumzika vya kutosha na hivyo mtu anapoamka huwa na nguvu za kufanya
shughuli zake kwa ufanisi
JALI AFYA YAKO
Afya yako ni muhimu sana
lazima uhakikishe unakuwa msafi kwa kuonga na kuvaa nguo zilizo safi, kula mlo
kamili hakikisha unajipenda mwenyewe kabla ya kuwapenda watu wengine, mara tu
unaposikia dalili za kuumwa basi fika kituo cha afya mara moja kwa ajili ya
kufanya vipimo mbalimbali vya mwili, ni lazima kujali afya yako kwanza epuka
tabia hatarishi ambazo zinahatarisha afya yako au maisha yako kwa mfano unywaji
wa pombe, uvutaji wa sigara, utumiaji wa madawa ya kulevya, ukahaba na
mengineyo mambo kama haya hatarishi haupaswi kujihusisha nayo. jifunze zaidi namna ya kuimarisha afya yako ya akili hapa
TUMIA MDA
WAKO WA ZIADA VIZURI
Unaweza ukatumia muda
wako wa ziada kufanya mambo ambayo yataweza kuburudisha akili na mwili wako kwa
mfano kucheza mpira, kutazama sinema, kwenda kuwatembelea ndugu na marafiki
n.k lakini pia waweza kuutumia mda wako
wa ziada kupumzika. Ni vyema kujitengenezea ratiba maalum ya vitu ambavyo
utakuwa unavifanya katika siku yako lakini pia ni lazima kujua kwamba muda wako
wa ziada utautumia kufanya kitu gani ambacho kitakuletea manufaa na kukufanya
ujisikie vizuri kiakili na kimwili pia.
NENO LA
MWISHO
Ni vyema kujali afya yako
na kuhakikisha kwamba mwili wako unakuwa imara kwa kushiriki mazoezi mbalimbali
lakini pia unapaswa kuzingatia mlo kamili na kuishughulisha akili yako kwa
kufanya kazi mbalimbali, jipende kwanza mwenyewe na kuwa nadhifu ndipo hapo
itakapokuwa rahisi kuwapenda watu wengine, kumbuka kwamba afya yako ya kiakili
na kimwili inapokuwa imara ndivyo itakavyokuwa rahisi kuweka malengo yako na
kuyafikia kwa haraka
SOMA ZAIDI KUHUSU
Mambo 10 kuyajua unapokua mtu mzima
Namna ya kujenga afya yako ya akili
Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwenye chumba

