MAMBO AMBAYO UNAPASWA KUYAJUA UNAPOKUWA MTU MZIMA
Wakati ulipokuwa mtoto ni
tofauti sana na unapokuwa mtu mzima, zipo changamoto nyingi ambazo unapaswa
ukabiliane nazo wewe kama mtu mzima, unahitaji kuwa na hekima ya kutosha ili
uweze kuishi na watu waliokuzunguka vizuri hapa nitaelezea vizuri mambo ambayo
wewe kama mtu mzima ni muhimu kuyajua na wakati mwingine hakuna mtu ambaye
atakwambia haya mambo
1.YUPO MTU
ANAEKUPENDA BILA KUJALI VILE ULIVYO
Katika maisha yako
utagundua kwamba wapo baadhi ya watu wanakuchukia bila sababu za msingi au
pengine wanaona wivu kutokana na mafanikio ambayo umeyapata lakini ukae ukijua
kwamba yupo mtu ambaye siku zote atakupenda na atafurahia mafanikio yako
2. NDUGU
ZAKO WANAWEZA WAKAWA MAADUI ZAKO WA KWANZA
Wewe kama mtu mzima
lazima ujue kwamba sio kila ndugu yako anafurahia maendeleo yako na mafanikio
unayoyapata wapo wanaojifanya wanakupenda na kukujali lakini ukionyesha dalili
za kufanikiwa ghafla wanaanza kuchukia na kuona wivu hivyo huanza kupingana na
jitihada zozote utakazokuwa unazifanya
3.KIPAJI CHAKO
HAKITAONEKANA MPAKA UKIFANYIE KAZI KWA BIDII
Yawezekana wewe una
kipaji Fulani lakini ukae ukijua kipaji chochote hakiwezi kuonekana mpaka
ukifanyie kazi pamoja na mazoezi ya kutosha mpaka pale utakapokuwa umebobea
ndipo hapo watu watakapoona kwamba waweza kufanya mambo yanayohusiana na kipaji
chako kiurahisi nao watasema kwamba unakipaji au umepewa kipawa na mungu lakini
ni lazima kwanza ukihangaikie
4.WATU HUWA
NA TABIA YA KURUDIA MAKOSA YAO YALE YALE
Asilimia kubwa ya watu
wameathirika na tabia Fulani ambazo sio nzuri na mara nyingi watu hujikuta wakifanya makosa hayo hayo siku
zote, hii ikiwemo matendo yasiyo mazuri na matukio, hii hutokana na kujizoeza
vibaya katika maisha yao
5. JIPENDE
MWENYEWE KWANZA
Kujipenda mwenyewe
humuongezea mtu ujasiri lakini pia kujithamini, huwezi kusema kwamba unampenda
mtu mwingine na wakati wewe mwenyewe haujijali, lazima ujipende mwenyewe kwanza
ndipo utasema unawapenda watu wengine, vaa vizuri,kula vizuri, jithamini vile
ulivyo, watu wengine wanapoona unajithamini ndipo hapo wataanza kuvutiwa na
muonekano wako na kutamani kukufahamu kwa undani
6.KADIRI
UNAVYOZIDI KUFANIKIWA NDIVYO UNAPASWA KUWA NA MTAZAMO CHANYA
Unapopandishwa cheo au
kutoka levo moja ya maisha na kwenda nyingine ni muhimu kufahamu kwamba lazima
uwe na mtazamo chanya kwa sababu sasa utakuwa unadili na watu wa aina
mbalimbali ili uweze kufanya nao kazi vizuri hupaswi kuwa mtu wa kumuwazia
mwingine vibaya kwa haraka, kama unatabia ya kuwaza mabaya juu ya watu wengine
basi ukae ukijua mambo mengi unayoyafanya watu wengine wanaweza wasikusapoti
kwa sababu watajua kwamba unawawazia mabaya hii hupelekea kuharibika kwa
mahusiano aidha ya kikazi, kirafiki au kibiashara.
7. WATU
WALIOFANIKIWA HUWA WAKATILI KATIKA UTENDAJI WA JAMBO
Hii ni kweli na nimuhimu
ujue kwamba watu wengi waliofanikiwa huwa hawajali mawazo ya watu wengine au
mtazamo wao, wao wanapoamua jambo basi jambo hilo ni lazima litekelezwe na ni
lazima wafanye juu chini ili kwamba dhamira yao iweze kutimia, hivyo ni muhimu
ujue kwamba kama wewe unahitaji kufanikwa katika mambo yako ni lazima kuwa na
tabia hii ya kuwa na ukatili katika utendaji si kwa ubaya bali kwa ukali
kuhakikisha kwamba jambo lako lazima lifanikiwe
8.LOLOTE
UTAKOLOFANYA LAZIMA KUNA WATU WATAKUCHUKIA
Kaa ukijua kwamba huwezi
kumfurahisha kila mtu, wapo watu ambao hata uwepo wako hawawezi kuufurahia jua
kwamba kuna watu ambao huchukia hata kama ukifanya jambo zuri la kusaidia
wengine au vyovyote vile utakavyofanya, hata sasa yupo mtu ambaye unaweza
ukamjua au usimjua anakuchukia tu namna unavyoongea,kutembea au unapofanya kazi
zako kwa hiyo ni muhimu kuwa makini sana hasa unapokuwa umetenda jambo zuri
usije ukahisi kila mtu amekufurahia
9.MAJUKUMU
HAYAEPUKIKI
Unapokua mtu mzima ni
vyema kujua kwamba hutaweza kuepuka majukuma asilimia mia hata kama ukisema
hutaoa au kuwa na watoto lakini bado utakuwa na majukumu katika familia yako
kama kusaidia wadogo zako and ndugu zako, huwezi eti kwa sababu wewe
umefanikiwa sana basi ukajitenga na ndugu zako kabisa hilo wala si jambo zuri
mbele za watu na mbele za mungu
10. KAZI
NDIO MSINGI WA MAFANIKIO
Hakuna njia nyingine ya
kufanikwa kiuchumi na kimaendeleo kazi peke yake ndio jawabu la mafanikio ya
mtu , mtu yeyote ambae ni mvivu wa kufanya kazi hawezi kamwe kuja kufanikiwa
katika jambo lolote analotaka kulifanya, bidii ya kazi itakufanikisha na
kukuridhisha moyo wako pale unapomaliza kazi yako , fanya kazi zako kwa bidii
sana na kwa ustadi wa hali ya juu nawe utayafurahia maisha unayoishi
SOMA
ZAIDI KUHUSU

