Msongo wa mawazo

 JINSI YA KUJIEPUSHA NA MSONGO WA MAWAZO

Kupatwa na msongo wa mawazo ni jambo ambalo kila mtu amelipitia au huwa linatokea mara kwa mara, kwa sababu ya shughuli mbalimbali ambazo tunajihusisha nazo hutusababishia mlundikano wa mawazo mbalimbali ndani ya vichwa vyetu, msongo wa mawazo huweza kuleta madhara mbalimbali ikiwemo maumivu ya kichwa, mtu kukosa uelekeo wa maamuzi lakini pia wapo watu ambao unaweza kuwaona hata barabarani wakiwa wanaongea peke yao kitu ambacho kinaweza kuwa ni cha ajabu mbele ya macho ya watu wengine, njia bora za kuthibiti msongo wa mawazo ni kama zifuatazo

KUFUNGA NA KUOMBA

Ningesema kufunga peke yako kusingekuwa na mantiki yoyote hivyo ni lazima kuomba pia, hii ni njia nzuri sana ya kuepukana na msongo wa mawazo,unapofunga unapaswa usamehe wengine,usiwe na hofu na kumwamini mungu, usikae na chuki au mawazo mabaya, kufungu humpa mtu displini ya hali ya juu na hivyo huweza kujikontrol kuanzia ufahamu wake na mwili wake kiujumla unaweza kufunga angalau siku mbili kwa wiki hii itakuwezesha kukaa wiki nzima bila kupatwa na msongo wa mawazo,mfungo huuwa nguvu ya maumivu ya moyo, chuki, huzuni, hofu n.k soma Zaidi mambo unayopaswa kufanya unapokuwa kwenye mfungo hapa

EPUKA KUTEMBEA UMBALI MREFU PEKE YAKO

Mtu anapokua anatembea mwenyewe peke yake hii huupa ufahamu wake uhuru wa kutafakari mambo mbalimbali kwa kina, mawazo huachiliwa kutoka kwenye ufahamu wako wa ndani(subconscious mind) na kuja mfululizo kama maji yanayotiririka baada ya mda utajikuta huna tena uwezo wa kukontrol mawazo yako, kama unatafuta wazo Fulani na ungependa kutafakari sana basi mbinu hii ya kutembea umbali mrefu itakusaidia kupata solution ya tatizo Fulani.

KUFANYA MEDITATION

Meditation kwa maneno ya Kiswahili ninaweza kusema ni kutulia sehemu na kutokuwaza au kufikiria jambo lolote,kuweka mawazo yako kwenye eneo moja tu ndani ya dakika 20 au 30 na kuendelea, mtu anapomaliza kufanya meditation hujisika vizuri na hupata tena uwezo wa kukotrol mawazo yake hivyo meditation ni nzuri kwani humrudishia mtu focas katika mambo ambayo anataka kuyafanya.

PATA USINGIZI WA KUTOSHA

Kutokupata usingizi mzuri kunachangia sana kumfanya mtu kuwa na msongo wa mawazo maana ubongo unakuwa umechoka pamoja na mwili hivyo hutaweza kutenda jambo lolote kwa ufanisi au ustadi, inashauriwa kwamba mtu anapaswa alale angalau masaa 7 au 8 kila siku, unapopata usingizi wa kutosha unaruhusu mwili wako pamoja na ufahamu wako kujitengenezea nguvu mpya ambayo itakusaidia kufanya shughuli zako pale utakapoamka, wakati mwingine watu hawapati usingizi wa kutosha kutokana na kusumbuliwa na madoto ya ajabu ajabu au ya kutisha hivyo ni muhimu kuwa na hekima ya namna kuepuka ndoto mbaya, soma Zaidi kuhusiana na ndoto hapa

MAZOEZI

Kufanya mazoezi ni mojawapo ya njia nzuri ambayo itakusaidia kuepukana na msongo wa mawazo badala ya kukaa peke yako ukiwa idle unaweza kutumia mda wako wa jioni kwenda kufanya mazoezi lakini pia mazoezi yanafaida nyinginezo nyingi ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kukupa afya njema ya akili  na kukongezea focus katika malengo yako ya kimaisha

EPUKA KUTAFAKARI SANA

Yapo matatizo mengi tunayoyapitia na tunahitaji kutafakari kwa mda ili tuweze kujua ni mbinu zipi tutazitumia kukabiliana nayo lakini kutafakari kwa mda mrefu huweza kusababisha hofu, mashaka hasa pale unapoona kwamba jambo lako halina ufumbuzi, hii hupelekea msongo wa mawazo  na mwisho mtu huanza kujisikia vibaya,kukosa furaha na kupoteza focus katika maisha yake hivyo tafakari kwa muda ukiona hakuna mafanikio endelea na shughuli nyingine kwanza baadaye unaweza hata ukamshirikisha na mwenzako au kuomba ushauri juu ya utatuzi wa jambo Fulani

JIWEKE HURU

Lazima uhakikishe unalinda ufahamu wako kutokana na mtazamo hasi, epuka mawazo mabaya, mawazo mabaya huweza kuumiza hisia zako kiurahisi na kukufanya kuwa mhanga wa mawazo hayo, mawazo mabaya huchangia mtu kuwa na hofu,wasiwasi, mashaka na hata kupelekea magonjwa mbalimbali ya moyo ikiwemo presha ya kupanda au kushuko, mshuto wa moyo n.k

NENO LA MWISHO

Jenga mfumo wa maisha yako vizuri, kuwa na mahusiano na watu vizuri ambao wanaweza wakakushauri namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha unazopitia, kula vizuri, upeka tabia zisizo na manufaa, fanya kazi kwa bidii na siku zote onyesha uwezo na nia ya kusaidia wengine hii itakusaidia pale siku na wewe utakapohitaji msaada watu wengine nao watakusaidia kwa sababu ya tabia yako kuwa nzuri

SOMA ZAIDI KUHUSU

Mambo 10 kuyajua unapokuamtu mzima

Namna ya kujenga afyayako ya akili

Jifunze kuhusu ndoto

Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwenye chumba

Mbinu za kupunguza uzito

 

 

 

 

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post