jinsi ya kujenga tovuti(website)

                                HATUA ZA KUJENGA TOVUTI

Kujenga tovuti kunasumbua kidogo haswa ikiwa hujawahi kujenga, na hata kama umeijenga, bado itategemea jukwaa(platform) ambalo umetumia ili kukamilisha malengo uliyonayo, ikiwa huna uzoefu na jukwaa unalotumia basi itabidi ujifunze, jinsi linavyofanya kazi ingawa watu wote wanaounda wavuti lazima wafuate hatua kama zilivyoelezewa hapa chini.

NAMBA 1. WEBSITE YAKO INATOA ELIMU GANI? (NICHE)

Ni muhimu sana kujua ni niche gani unataka kuzingatia, ikiwa utaunda tovuti basi jiulize tovuti hiyo inahusu nini, na inajaribu kufikia nini kuna niche kadhaa ambazo unaweza kuchagua. kwa mfano unaweza kuchagua niche ifuatayo kama vile afya na utimamu wa mwili, elimu, mitindo na muundo, fedha za kibinafsi na uwekezaji, kuuza bidhaa, uuzaji wa kidijitali, kublogi na kutengeneza pesa mtandaoni, mafunzo, kuuza kozi ya mtandaoni au inaweza kuwa tangazo lako la kampuni yako au taasisi yako.

NAMBA 2. KUNUNUA JINA LA WEBSITE (DOMAIN)

Kabla ya kuanza kutengeneza tovuti yako lazima ununue jina la tovuti yako, kabla hujanunua domain, jina la website au blog yako linaweza likasomeka kama ifuatavyo www.worldissuez.blogspot.com lakini ukishanunua domain sasa litabadilika na kuwa www.worldissuez.com.  neno blogspot litaondolewa kutoka kwa domain yako kwa kuwa wao ndio wamiliki wa kwanza wa jina hilo, kuna aina tofauti za domain wengine huishia na .com, .net, org, tech na kadhalika, unaweza kununua domain kwa Hostinger, Hostgator, godaddy, Bluehost, Namecheap, DreamHost

NAMBA 3. NUNUA HOSTING

Sasa hii ndio inaleta tofauti kati ya website na blog ambapo kwa blog hakuhitaji kununua hosting, ukishanunua domain basi unaweza kuanza kutengeneza blog yako lakini website inahitaji domain na hosting na kila moja inakuja kwa bei tofauti kulingana na mahali uliponunua, unaweza kununua hosting aidha kwa mwezi, miaka au miaka miwili na kadhalika, watu wanaohost website ni wale wanaokupa nafasi ya kuhifadhi data zako na kuwezesha tovuti yako kuonekana duniani kote, huku domain ni jina tu la tovuti yako, unaweza kununua domain pamoja na hosting kwa hostinger, hostigator, godaddy, bluehost, Namecheap,DreamHost na kadhalika.

NAMBA 4. CHAGUA JUKWAA(platform)

Kuchagua ni jukwaa gani unafaa kutumia kuunda tovuti yako ni muhimu sana kwa sababu baadhi ya watu wangependelea zaidi jukwaa fulani kuliko nyingine, anaetengeneza  tovuti anaweza kuamua jinsi tovuti yake itakavyokuwa kutokana na ubora au uzuri wa platform ambao mtu huyo anaitumia kutengenezea tovuti hiyo baadhi ya platform ni WordPress, Wix, Squarespace, Shopify, au GoDaddy,, weebly

NAMBA 5. KUCHAGUA MUONEKANO(Theme)

Mandhari ya tovuti yako ni muhimu sana, muonekano wa tovuti yako ni muhimu, hii ni sababu mojawapo ya kuwapa watu  uwezekano mkubwa wa kusoma na kukaa muda mrefu katika tovuti ambayo inaonekana nzuri na ya kuvutia, changuao muonekano mzuri wa kitofauti unaweza kuchagua mandhari ambayo ni bora Zaidi, kwa afya na usawa, biashara na fedha, uuzaji wa washirika, shughuli za kijamii na kadhalika

NAMBA 6. ANZA KUBUNI

Baada ya kuchagua mada unayoipenda basi unaweza kuanza kuunda wavuti yako kulingana na matakwa yako, tengeneza tovuti ambayo sio ngumu sana kuilewa kwa mtumiaji na inapaswa kuonekana ya kuvutia, nitaorodhesha sifa zingine za wavuti bora ambayo unaweza kubuni.

          i) Muonekano mzuri

Tovuti yenye muonekano mzuri inaweza kuvutia watumiaji wapya,kila mtumiaji wa tovuti huvutiwa na tovuti ambayo imeandikwa vizuri na ina mpangilia mzuri wakati anaposoma jambo fulani

           ii) Urahisi wa kutafuta jambo

Tovuti lazima iwe rahisi kuitumia ikiwa mtumiaji atahitaji kujua jambo Fulani basi atalipata kwa urahisi kwa mfano mtumiaji anaweza kutaka kujua jinsi ya kuwasiliana na mmiliki wa wavuti basi atafute maelezo hayo kwa urahisi kwenye wavuti yako.

           iii) Taarifa nyingi

tovuti nzuri lazima iwe na taarifa za kutosha, lazima ujaze maelezo ya kutosha kulingana na topics ambayo umechagua, hii itawawezesha wasomaji mbalimbali kutembelea tovuti yako katika muda mwingi kutafuta taarifa fulani.

         iv) Picha zenye ubora wa juu

katika tovuti yako lazima utumie picha za ubora wa hali ya juu sana kuna tovuti nyingi ambazo unaweza kwenda kupata picha hizi ambazo zina ubora wa hali ya juu bila malipo kama vile pexel, unsplash, pixabay, freeimages, pikwizard

NAMBA 7. ANDIKA POST ZAKO KWA UFASAHA

Ukishamaliza kutengeneza muonekano wa website yako basi itabidi uandike post, unaweza kuchagua kuchapisha kurasa zako kisha utapost halafu utaendelea kutengeneza website yako mpaka iwe vile vile ulivyotaka, lazima ujifunze kutumia heading zinazovutia kwenye yako ili kuvutia msomaji

NAMBA 8. SHARE LINK YAKO

Unaweza kuchagua kushare link ya tovuti yako au post yako ili watu waje kuitembelea, lakini baada ya mda fulani tovuti inapojulikana sana na ina taarifa nyingi watu wanaweza kuipata kwenye google search, lakini njia ya awali ni kushare link na watu ikiwa na heading nzuri ili kuvutia watu wengi zaidi kuja kutembelea tovuti yako hapa

USHAURI WA MWISHO

Tovuti au blogu yako lazima iwe na kurasa muhimu kwenye upande wa menyu, hakikisha kwamba kurasa zifuatazo zinaweza kuangaziwa kwa urahisi kuhusu ukurasa wetu(about us), wasiliana nasi (contact us), sera ya faragha(privacy policy), kanusho(disclaimer), sheria na masharti(term and condition) haya ndiyo yanayotoa maagizo au sheria mtu yeyote ambaye anataka kutumia yaliyomo kwenye tovuti yako kwa ajenda zao wenyewe

Post a Comment

Previous Post Next Post