Afya ya akili

 

JINSI YA KUBORESHA AFYA YA AKILI

Afya ya akili ni nini?

Afya ya akili ni hali ya ustawi wa kifikra inayomwezesha mtu kukabiliana na mazingira yake, kuwa na hisia bora, akili isiyo na msongo wa mawazo, furaha, kutokuwa na wasiwasi na kadhalika hizi ni sababu zinazochangia afya njema ya akili, ingawa afya ya akili ni muhimu sio kila mtu ana afya njema ya akili baadhi ya watu wanapata ugumu na changamoto mbalimbali za maisha na hivyo kuathiri hali zao za kiakili lakini pia kutokana na aina mbalimbali za magonjwa ambayo mtu anaweza kuyapata au kuumia maishani hali ya afya ya akili inaweza kuathirika.

Lakini hata hivyo kuna njia ya kuboresha hali ya afya ya akili katika maisha moja, ikiwa mtu huyo atakuwa na bidii kufuata maagizo yote yaliyotolewa na mtoa huduma wa afya ya akili au daktari.

Jinsi ya kuboresha afya ya akili?

Hapa kuna baadhi ya mambo ambayo mtu anaweza kufanya ili kuboresha hali yake ya afya ya akili

KULA MLO KAMILI

Mlo kamili ni aina ya chakula chenye virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika mwilini, ulaji wa chakula chenye madini, vitamini, protini, wanga n.k ni muhimu sana kwani vyakula hivi vinachangia sana afya ya mwili na akili pia, virutubisho hivi vitaupa mwili nguvu na kumwezesha mtu kufanya shughuli zake kwa ufanisi

Epuka kutumia kafeini kupita kiasi, sukari, vyakula vya kukaanga, vyakula vyenye viungo vingi na pombe kwa sababu ni hatari kwa mwili ambao kinga yake tayari ni dhaifu.

Lishe iliyokamilika husaidia kudumisha uzito bora wa mwili, lakini pia hupunguza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya muda mrefu kama saratani, kisukari, unene, shinikizo la damu na magonjwa mengine yanayotishia maisha.

Baadhi ya vyakula huimarisha hali ya kiakili na kuongeza afya ya akili kwa mfano kula samaki kumeonekana kuongeza uwezo wa akili wa mtu(intelligent quotients).

FANYA MAZOEZI KILA SIKU

Kufanya mazoezi ni muhimu sana, mazoezi yanaufanya mwili mzima kuwa na afya na uchangamfu, inashauriwa mtu afanye mazoezi angalau dakika 20 hadi 30 kwa siku, mazoezi yanaweza kusaidia kuboresha afya ya akili ya mtu.

Kuna aina tofauti za mazoezi ambayo mtu anaweza kufanya kwa mfano mazoezi ya anaerobic, yoga au kufanya shughuli za nguvu kama sehemu ya mazoezi lakini bora zaidi ni kwamba mtu lazima afanye mazoezi ya kuchangamka(anaerobic) kama kukimbia, kuruka, kucheza, kuendesha baiskeli na kadhalika,

Kwa mfano, mtu anapokimbia huruhusu mzunguko wa damu katika mwili wake wote ikiwa ni pamoja na kwenye ubongo wake, hii huongeza utendaji kazi wa ubongo kwani damu inaweza kufika sehemu zote za ubongo.

JITHAMINI

Lazima ujitendee mwenyewe na wengine kwa heshima, epuka kujichanganya na mambo yote ambayo yatakufanya ujisikie vibaya, moja ya tabia kubwa ya watu waliofanikiwa ni lazima ujifunze kujipenda, weka malengo yako juu na kuyafuata, hii itakuongezea kujiamini,kujipenda,kuwa na bidi kwa ujumla huimarisha mfumo mzima wa jinsi utavyofikiri na kuimarisha afya yako ya akili

KUNYWA MAJI MENGI

Inashauriwa kuwa ni lazima mtu anywe maji mengi ili kuuwezesha mwili kufanya kazi vizuri, maji yanauwezesha mwili kulainisha sumu kali mwilini kwa ajili ya kuzitoa nje, hii huchangia katika kufanya afya yako ya akili kuwa nzuri na imara.

ONDOA MSONGO WA MAWAZO

Kwa kawaida msongo wa mawazo huja na kuondoka jambo ambalo ni hatari ni kuruhusu msongo wa mawazo uendelee kukutesa . Kuwa na mawazo na wasiwasi mwingi sio nzuri kwa afya yako, kwa hivyo tumia mbinu za kupunguza msongo wa mawazo kama meditation, jifunze ukimya unapokuwa peke yako ambapo unaruhusu akili yako na mwili wako kupumzika kwa dakika chache bila kufikiria chochote, yoga na kadhalika. Ili kuboresha hali yako ya kiakili ni lazima akili yako isiwe na wasiwasi, woga, mawazo mengi jifunze kukuweka huru kiakili.

FANYA MAMBO YANAYOKUPA FURAHA

Jitahidi kufanya mambo ambayo yatakupa furaha katika maisha yako, fanya vitu ambavyo unavipenda sana, hii itaondoa nafasi ya kupata msongo wa mawazo, hofu na wasiwasi.

Wakati fulani kufanya kile unachopenda hufanya akili yako kuwa huru, yenye afya na inakupa furaha

ACHA TABIA YENYE MADHARA

Tabia mbaya kama kuvuta sigara, unywaji pombe sio nzuri kwa afya yako ya akili, jifunze kujishughulisha na mambo mazuri ya kimaadili

Tabia mbaya inaweza kuharibu sio tu hali yako ya kiakili lakini pia afya yako ya mwili, unaweza ukajikuta unaanza kuugua kwa sababu tu za uvutaji wa sigara, bangi au ukapata matatizo ya kiafya zaidi.

WEKA MALENGO HALISI

Epuka kuchanganyikiwa na mambo yanayoweza kukupa matumaini ya uongo jifunze kujiwekea malengo yenye uhalisia Malengo unayojiwekea lazima yawezekane na kufikiwa. Fanya kazi ili kufikia malengo yako, soma vitabu zaidi, jifunze kutoka kwa wengine, daima uchangamshe ubongo wako kwa maarifa zaidi. Acha uvivu na usiwe mlalamikaji fanya bidii ili kuboresha kiwango chako cha maisha kwa ujumla

SOMA ZAIDI

Jifunze vyanzo vya ndoto mbaya

Jinsi ya kuwa tajiri

Aina tano za miili

Jinsi ya kumjua nabii wa uongo

Kwa nini maisha magumu

Jinsiya kupunguza uzito

Mambo ya kufanya kwenye mfungo


Post a Comment

Previous Post Next Post