SOFTWARE ZINAZOTUMIKA
ZAIDI KWENYE VISUAL EFFECTS
Unapoingia katika tasnia ya filamu, muziki au games kama mhariri au msanii kujua ni programu gani ya kutumia ni muhimu sana hii itakuwezesha wewe kutumia programu inayofaa katika kazi yako, kama wewe ungependa kujifunza visual effect kiujumla ni lazima ujue baadhi ya program muhimu kama zifuatayo
SOFTWARE KWA AJILI YA
3D
Kama artist wa visual effects lazima uwe na ujuzi na software angalau moja ambayo inahusika na kutengeze three dimension objects (3D), kwenye 3D kuna ujuzi wa kufanya utengenezaji wa shepu za vitu(modeling), kukitengenezea kitu ulichokifanya nyenzo ili kuweza kuonyesha mjongeo (rigging), mjongeo(animation),kuweka rangi au muonekano wa object yako(texturing), kutengeza vimiminika,milipuko,moshi na nakadhalika(simulation) na mengineyo basi lazima ujifunze programu moja au mbili kati ya zifuatazo.
3D Maya ni programu bora zaidi ya 3d kwa kweli ni programu inayoongoza kwenye movie industry na hata game industry, imetumika sana katika kutengenezea sinema za Hollywood kwa muongo mmoja sasa, kila mtu ambaye ana hamu ya kuingia kwenye ujuzi wa 3D lazima ajifunze kuifahamu sana hii program, kampuni nyingi za sinema huajiri haraka watu ambao wana uzoefu wa kutosha wa kutumia programu hii, hii ni zana ambayo inatumika sana katika kufanya mambo ambayo ni mazuri na ambayo yatapunguza gharama katika movie au game.
Houdini ni programu ya 3D inayotumiwa zaidi na wataalam, Houdini ndiyo program ambayo ni ngumu kidogo kujifunza kwa anayeanza lakini programu hii inaweza kufanya karibu kila kitu ambacho msanii wa 3D anatamani, Houdini pia inatumika kutengenezea plugin kwa ajili ya program zingine za 3d, Houdini inajulikana zaidi kwa kutengeneza uharibifu(destructions), kampuni nyingi zimeamua kubadilisha utendaji wake wa kazi kutoka kwenye program ya maya na kuhamia kwenye Houdini polepole, kwani ni program yenye nguvu ambayo inaweza kutumika katika filamu, games, picha za mwendo na kila aina ya usanifu.
Blender
ni program ambayo ni ya bure, maana yake ni kwamba msanii yeyote anaweza
kuitumia katika kazi yake hata kama hana hela ya kwenda kununua 3d software,
mtu yeyote anaweza tu kuingia kwenye tovuti ya blender na kuipakua, programu
hii inapendwa na wasanii wengi kwani ina zana zote za kufanyia kazi zako za 3D
kwa ufanisi wa hali ya juu. Blender haijaainishwa kama programu ambayo tasnia za
games na movies zitaipa nambari moja linapokuja suala la kazi ya 3D.
Cinema 4D program ambayo ni rafiki sana, ina muonekano mnzuri na ya kuvutia, hii inatumika zaidi katika eneo la picha ya mwendo(motion graphics) ni rahisi sana kuitumia, mtu yoyote anaetaka kujifunza 3D basi Cinema 4d itamfaa ili kumpatia ujuzi wa awali Cinema 4D inatumika sana katika filamu, games, muziki, matangazo na kadhalika.
Hii Zana(program) bora na ya kushangaza ya 3D, hufanya kazi nzuri na za kupendeza, 3D max ndiyo zana bora zaidi ya utengezaji wa vitu vya 3D, studio nyingi hutumia program hii, 3d s max inatoa uwanja mpana kwa msanii katika kutengeneza mambo mbalimbali ya games au movies pamoja na animation.
Z
BRUSH hutumiwa na wasanii mbalimbali kwa ajili ya uundaji wa vitu vya 3D (3D
modeling and sclupting), msanii atafanya kazi yake katika z brush na kuihamisha
katika programu nyingine kama Maya kwa uhuishaji, ikiwa unajishughulisha na uundaji
wa vitu vya 3D basi Z BRUSH ndiyo software bora kwa ajili ya hiyo kazi.
KUCHANGANYA
ELEMENT(COMPOSITING)
Hii ni sanaa ya kuchanganya vitu tofauti ili kuleta picha moja ya maana na ya uhalisia hapa pia zipo program mbalimbali ambazo artist anaweza akazitumia kukamilishia kazi yake, mfano wa program hizo ni kama zifuatazo
Ni programu inayotumika sana katika tasnia ya sinema, ni ngumu kidogo kujifunza lakini kama una bidii ni rahisi kuelewa na kuitumia, programu hii ni ya kushangaza na uwezo wake ni mkubwa, ni programu ya msingi na inatumia kitu kinachoitwa node base system, NUKE inatumiwa sana katika kutengenezea filamu, games, n.k.
After
effects ni zana bora kwa ajili kufanya motion graphics,inaweza kutumika
kutengeneza movies, after effect ina uwezo mkubwa na ni bora zaidi kwenye
kutengeza motion graphics kwa ajili ya matangazo mbalimbali, sio ngumu
kujifunza,kama unapenda motion graphics basi after effect ndio mahala pake.
hii
ni software kama nuke ambapo na yenyewe hutumia mfumo wa node kwa ajili ya
kufanya editing ambapo humpa msanii nafasi ya kutunga na kuziletea uhai picha
zilizokufa(still images), , ikiwa unajua jinsi ya kutumia nuke basi fume
effects pia itakuwa rahisi kuielewa
KUHARIRI VIDEO
Premiere Pro ni program ambayo hutumika kuedit video, vipande vya video huunganishwa ndani ya premier pro kwa ajili ya kutengeneza video moja, adobe Premier pro ina zana zote ambazo msanii anaweza kutamani kuwa nazo, unaweza kufanya kazi nzuri unapotumia programu hii, Premiere inatoa zana zote zikiwemo zana za rangi, pia premier pro hushirikiana na adobe encore kwa ajili ya kumsaidia msanii kutengeneza aina ya video anayoitaka kama ni ya kwenye simu, youtube nakadhalika
ni program nzuri ya kukata, kuhariri video na kuingiza sauti, wahariri ambao wana uzoefu wa kufanya kazi na aina hii ya programu wanaweza kuifurahia kwa sababu ina zana karibu zote za kufanya kila kitu ambacho mhariri anaweza kutamani, program ya final cut pro hufanya kazi kwenye kompyuta za apple, Kwa hivyo kwa bahati mbaya ikiwa huna kompyuta ya apple basi huwezi kutumia aina hii ya program
Program
ya sony vegas ilikuwa inajishughulisha na uhariri na utunzi wa sauti pekee
lakini baadaye wakaongeza jukwaa la toleo la video, ni program ambayo ningependa kila msanii anayetaka, kuweka sauti kwenye
video yake basi atumie sony vegas
Programu
hii ina vitu vyote ambavyo msanii atahitaji, inatumiwa katika kuhariri video,
lakini pia ina uwezo wa kupakia video moja
kwa moja kwenye YouTube mara tu baada ya kazi yako ya uhariri itakapokamilika.
PICHA
Katika
eneo hili ADOBE PHOTOSHOP ni bora zaidi linapokuja suala la uhariri wa picha,
adobe Photoshop ina karibu kama sio zana zote ambazo msanii anaweza kuzitumia
kufanya chochote anachotaka, lakini pia ADOBE ILLUSTRATOR inaweza kusaidia
katika kuhariri na kubuni picha za 2D, adobe illustrator hutumiwa zaidi na
wasanii ambao wanapenda kutengeza logo mbalimbali
UTENGENEZA WA
VIMIMINIKA (FLUID SIMULATION)
utengenezaji wa vimiminika unaweza kufanywa katika baadhi ya programu za 3D kama MAYA, HOUDINI na BLENDER lakini kuna program ambazo ni maalum sana kwa kutengenezea vimiminika kama maji,uji, asali n.k ambayo inaitwa REAL FLOW programu hii ina kila kitu kinachohitajika ili kutengeneza kimiminika cha aina yoyote.
SOMA
ZAIDI KUHUSU

