jifunze kuhusu ndoto


NDOTO MBAYA NI NINI? NINI HUSABABISHA? NA JINSI YA GANI YA KUZIEPUKA?

Unapolala usiku unaweza kuona vitu ambavyo vinaweza kusumbua sana akili yako na moyo wako vitu hivi vinaweza vikawa vya kutisha, kuchukiza, kushtua na pia vinaweza kukatisha tamaa lakini aina hizi za ndoto huchochewa na kitu fulani katika maisha ya mtu, ndoto mbaya inaweza kumjia matu yeyote wakati akiwa amelala na wakati mwingine ndoto mbaya inaweza kutuonya juu ya jambo fulani ambalo linaweza likatokea katika siku za usoni.ndoto hudhihirika katika mifumo tofauti ya maono na wakati mwingine elimu ya kuhusu maono huitajika kuna miili tofauti inayotumika kwenye maono ya usiku bonyeza hapa kujifunza aina za miili

Hata hivyo, ndoto hazitokei tu, ndoto husababishwa na mambo fulani ambayo tunayafanya katika maisha yetu kwa mfano watu ambao tunakutana nao, mahali tunapokwenda, mambo ambayo tunatazama, mambo ambayo tunafikiri na kadhalika.

Endapo kama hupendi kabisa kuota ndoto yoyote mbaya wakati wa usiku na unataka kupata usingizi mzuri sana, wa amani usiku basi kuna baadhi ya mambo mbalimbali ambayo wengi hawayajui kuhusu ndoto, kwa sababu watu wengi hawana ujuzi wa ndoto, Hebu tuone mambo ambayo yanaweza kusababisha ndoto mbaya

MATENDO/MATUKIO MABAYA

Ukishiriki tendo au matukio mabaya unaweza ukaanza kuota ndoto mbaya matendo hayo mabaya uliyoyafanya huweza kuja  kama ndoto mbaya yakijielezea katika ndoto nini maana ya ulichokifanya, uwakilishi wa ulichofanya/unachofanya au unatarajia kukifanya utakuja kwenye ndoto zako hii inakupa fununu ya jinsi ukubwa wa madhara ulivyo

Shughuli zote hizi tunazozifanya aidha ni nzuri au mbaya tayari zimesemwa katika kanuni za MUNGU na baadhi yake zinaweza kuelezewa na binadamu wa kawaida kulingana na mwenendo wa maisha kwa mfano kuua kamwe si jambo zuri hauitaji kwenda shule kujua hilo.

KULALA NA NGUO/SHUKA CHAFU

Ninaposema najisi maana yake ni kitu ambacho ni kichafu kiroho ukipatwa na ndoto mbaya jambo la kwanza ningekushauri ufanye ni kuvua nguo ulizovaa na kubadilisha shuka baadhi ya nguo tunazokuwa nazo tayari zimetumika katika shughuli mbaya. kabla hazijatufikia hivyo unapolala roho yako inachanganyikana na nguvu zilizoko ndani ya nguo au shuka ambayo unatumia hivyo utaweza kuona baadhi ya matukio yaliyowahi kufanywa na mtumiaji wa nguo hiyo au shuka hiyo, nguo au shuka hutunza kumbukumbu za matukio ya watumiaji wa vitu hivyo, maombi hayawezi kuondoa ndoto hizi mbaya bali huondoa tu hofu ndani yako lakini ukirudia kulalia vitu hivyo utapata ndoto za namna hiyo hiyo.

Kwa usingizi mzuri wa usiku inashauriwa kununua nguo mpya ambayo haijawahi kutumika hapo awali au kwenda kwa fundi cherehani na utengeneze nguo yako mwenyewe na shuka hii itakuwezesha kuepuka kumbukumbu zote mbaya za matukio ambazo zimerekodiwa katika nguo.

KULA CHAKULA CHA UCHAWI/MANUWIZO

Ikitokea umekula kitu chenye uchawi hakuna unachoweza kufanya utaota ndoto mbaya usiku kucha hata ukiomba haitafanya kazi maana chakula hicho kipo ndani yako, utakoota ndoto namna hiyo mfululizo na unajua umekula sehemu Fulani ambayo una mashaka nayo basi kaa macho usilale mpaka asubuhi mpaka pale ambapo chakula hicho kimeyeyuka na kutoweka kabisa mwilini mwako.

Sehemu zingine ambazo tunaenda kula sio za kuaminika, jitu linaweza kuweka kitu kwenye chakula kwa ajenda zake zisizojulikana na inapotokea umekula hicho chakula basi ile nguvu mbaya itajidhirisha kwako wakati wa usiku ambapo ndipo ambapo unaweza ukaona vitu vya kishetaji ukiwa umelala hivyo hakikisha mahali unapoenda kula ni salama, safi na pa kuaminika

KULALA BILA KUOMBA

Usipoomba halafu ukalala ina maana kwamba huna ulinzi wa ziada, maombi kabla ya kulala ni muhimu sana kwani unapoomba roho za kishetani haziwezi kukupata kwa sababu zinachukia chochote kinachohusiana na maombi.

Ni vyema kusoma neno la Mungu kabla ya kulala na kumkaribisha Mungu akulinde na mabaya yote yanayotokea usiku. Unapoomba na kumkaribisha Mungu nafasi ya pepo wachafu kukupata ni ndogo au sifuri hii itakupa usingizi mzuri wa usiku.

Na unapoomba funga ubavu wa kushoto, kulia , juu na chini aina za ndoto pia husabishwa na ubavu uliolalia kujifunza kuhusu ubavu nitaelezea kwenye Makala nyingine

KULALA BILA KUOGA

Kuoga ni muhimu sana kabla ya kulala, hii ina maana kwamba unaondoa nguvu zote zilizokung'ang'ania, ulipokuwa bize kazini ulikutana na watu wa aina mbalimbali na kuchangamana nao baadhi ya watu hao hukuachia nguvu au nishati hasi wengine nishati chanya kwa hivyo kuoga ni njia rahisi ya kuondoa nishati/nguvu yoyote iliyoambatanishwa na wewe

Hapo zamani za kale walitumia maji safi na chumvi kusafisha nguvu zote hasi zinazozunguka mwili na kukuacha msafi, kulala na nguvu zisizo zako hupelekea kuota ndoto usiku usizozijua na chanzo cha nishati kikiwa kibaya basi wewe utaota ndoto mbaya 

KUANGALIA FILAMU FULANI ZA KUTISHA

Kuangalia filamu zenye matukio ya kutisha au matukio mabaya kunaweza kusababisha ndoto mbaya kwa sababu kwa kawaida televisheni inaweza kuchangia ndoto zetu, hivyo ikiwa unachotazama ni mambo ya kutisha basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata ndoto za kutisha ndoto hizi ni marudio ya mambo ambayo umekuwa ukiangalia.

Jinsi ya kuepuka ndoto mbaya

Kuoga kabla ya kwenda kulala

Kuoga itakusaidia kukaa safi na kuondoa nishati zote hasi zinazokuzunguka

Acha kutazama filamu ya kutisha

Tazama tu sinema za kawaida, filamu ya kutisha sio nzuri haswa kwa watoto, ikiwa hutaki kupata ndoto mbaya wakati wa usiku basi acha kutazama sinema za kutisha.

Nunua nguo mpya ya kulalia na shuka

Ni bora utafute nguo mpya ya kulalia na shuka yake lakini hakikisha kitambaa ambacho hakijawahi kutumika hapo awali, nguo yoyote iliyotumika itakuletea maono ya matukio aliyoyafanya mtumiaji wa kwanza na wala hizo ndoto hazina uhusiano na wewe, ikiwa nguo ni najisi basi utaota ndoto mbaya, kama sivyo basi pana tukio fulani ambalo lilifanywa na mmiliki wa awali wa kitambaa hicho

Acha kufanya maovu

Acha matendo yako maovu yanadhuru wengine, ni bora zaidi wewe na kutenda mema kwa jamii kuliko kuidhuru.

SOMA ZAIDI KUHUSU

Jinsiya kuwa tajiri

Aina tano za miili

Jinsiya kumjua nabii wa uongo

Sifaza mtu aliyefanikiwa

Jinsiya kuondoa harufu mbaya kwenye chumba

Post a Comment

Previous Post Next Post