TABIA ZA MTU ALIYEFANIKIWA
Mtu yeyote ambaye
amefanikiwa katika maisha huweza kuonyesha tabia mbalimbali ambazo watu wote
waliofanikwa huwa na hizo tabia hivyo ni muhimu kuzijua kama wewe ni miungoni
mwa watu ambao wangependa kufanikwa katika maisha haya, tabia hizo zikiwemo
WEKA
MALENGO MAKUBWA
Watu ambao wamefanikiwa
waliweka malengo makubwa na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba
jambo ambalo wamelipanga linakamilika, usipokuwa na malengo na ukakosa mpango
kazi basi ujue ya kwamba hautaweza kujua uelekeo wa maisha yako, unapaswa
kuweka malengo yako juu na mpango wako wa namna utavyoweza kufikia malengo hayo
MUONEKANO
Watu waliofanikiwa huwa
na muonekano mzuri hapa namaanisha namna wanavyovaa, watu waliofanikwa
hujipenda sana na kujali namna taswira yao inavyoonekana katika jamii
inayowazunguka, inawezekana wapo baadhi ya watu waliofanikiwa ambao wana
muonekano ambao ni simple lakini wengi wao huwa na muonekano wa kuvutia kuanzia
uvaaji,mahali pa kuishi, n.k ikumbukwe kuwa taswira ya mtu katika jamii au kazi
ndiyo itakayomsaidia kuheshimika au kudharaulika
TABIA
Mtu yeyote aliyefanikiwa
huwa na tabia nyingi nzuri kuliko mbaya kwa mfano tabia za unywaji pombe kupita
kiasi huweza kuleta madhara ya umaskini wa haraka kwa mtu wa hali ya kawaida,
zipo tabia nyingine nyingi ambazo sio nzuri na hazipaswi kumilikiwa na mtu
huyu, watu waliofanikwa hupenda kufanya kazi,kujifunza,kuwekeza nk, mtu yeyote
aliefanikiwa na lazima awe na mtazamo chanya na uwezo wa kukabiliana na
changamoto mbalimbali katika maisha ya kila siku, kwa hiyo ni vyema
kutojihusisha na tabia hatarishi kama uvutaji wa madawa ya kulevya, wizi,
ubakaji n.k soma Zaidi kuhusu tabia hatarishi hapa
MAHUSIANO
MAZURI NA WATU
Ili uweze kufanikiwa ni
lazima uwe na mahusiano mazuri na watu wengine au watu ambao unashirikiana nao,
mahusiano mazuri huweza kuwafanya watu kukushirikisha pale ambapo jambo Fulani
linapotokea ambalo kwa upande mmoja au mwingine linaweza kuwa na faida kwako
KUONGEA
Moja wapo ya maeneo
muhimu sana katika mafanikio ni kujifunza kuongea na kuelezea mambo kwa undani,
ni vizuri kujifunza kutoa ushauri, kutoa mawazo yako pale ambapo yatahitajika,
jifunze kuongea kwa kujiamini mbele za watu.
BIDII
Katika kila jambo ambalo
unaona limefanyika na kufanikiwa ni kwa sababu kuna watu wamefanya sana bidii
kuhakikisha kuwa jambo hilo linafanikiwa,mtu yeyote aliyefanikiwa ni mtu mwenye
bidii mno na hufanya kazi kwa masaa mengi tofauti na ratiba za kazi za kawaida,
hivyo ni vyema kujua kwamba watu waliofanikiwa wana mda mchache wa kulala,kusharehe
na kujihusisha na tabia za anasa wengi huwa na msongo wa mawazo ambao
unahusiana na kukamilisha kazi wanayoifanya
WEKEZA
Ni lazima kujifunza
kuwekeza pesa, pesa ndio kila kitu hivyo ni muhimu kupata maarifa ya fedha na
namna pesa inavyopatikana, ukiwa na pesa za kutosha itakurahisishia kufanya
shughuli zako nyingine bila kuwa na wasiwasi kuhusu pesa, mtu aliyefanikiwa
huwa na pesa nyingi na zingine akiwa ameziwekeza zikiendelea kujizalisha.
KUJIAMINI
Kujiamini ni muhimu sana
ni lazima mtu ajiamini yeye mwenyewe kabla ya watu kumuamini, unapofanya mambo
yako kwa kujiamini hufanya watu wengine kutamani kushirikiana na wewe katika
mambo mbalimbali hii itapelekea kuonekana katika jamii kwamba wewe ni mtu
makini na unaeweza kukamilisha mambo yako kwa wakati
NENO LA MWISHO
Watu wengi waliofanikwa
huwa ni wapambanaji na wana malengo makubwa katika maisha yao hivyo hufanya juu
chini ili kuhakikisha kwamba yale yote ambayo wameyakusudia yanatimia, ni vyema
pia wewe kama mtu ambae unatafuta
kufanikiwa kuhakikisha kwamba unaweka urafiki wa karibu na mtu aliyefanikiwa
ili kujua namna anavyofanya mambo yake ili uweze kujifunza Zaidi
SOMA ZAIDI KUHUSU
Namna ya kukabiliana na msongowa mawazo

