SIFA ZA MTU ALIYEFANIKIWA
Mtu yoyote ambaye
amefanikiwa katika maisha yake huonesha sifa mbalimbali ambazo watu wengi ambao
wamefanikiwa huwa nazo
Hapa nitaelezea sifa za mtu ambae ana tabia za watu ambao wamefanikiwa katika maisha yao
MUONEKANEKANO WAKE
Mtu yoyote ambae
amefanikiwa katika maisha yake ni lazima awe na muonekano mzuri na
ninapozungumzia muonekano ninamaanisha ni namna anavyovaa, mtu aliyefanikiwa
anavaa mavazi mazuri yanayovutia , mavazi mazuri huonesha kwamba mtu huyo
anajijali na anajipenda
Lakini pia muonekana wa kimwili kama ni
mwanaume lazima awe mwenye nguvu na imara,hivyo kama wewe ni mwanaume ni lazima
ujenge tabia ya kufanya mazoezi,mwanaume yoyote lazima awe na muonekano wa mtu
aliye imara
Lakini kama ni mwanamke
lazima awe na uzuri unaovutia mwanamke ni lazima ajali muonekano wake, shepu
yake, nywele zake,hivyo ni muhimu sana kwa mwanamke kujipenda na kujithamini
PESA
Mtu yoyote aliyefanikiwa
ni lazima awe na pesa lakini si pesa tu ni lazima awe na mifumo thabiti ya
kutengeneza pesa, hivyo mwanaume anapaswa afanye kazi kwa bidii ili aweze
kutengeneza pesa za kutunza familia au kufanyia mambo yake,
Mwanaume ni lazima
ujifunze kuwekeza pesa zake kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za
kimaisha, na hata mwanamke lazima ajue ni namna gani anaweza kujipatia kipato
kwa kufanya kazi kwa bidii kazi ambayo itampa heshima mbele za watu
Wapo watu mbalimbali hapa
duniani ambao tunaweza kuwachukulia kama maroll model katika maisha yetu
wamefanikiwa na wanajipenda lakini pia wanapenda kazi wanazozifanya
PENDA UNACHOKIFANYA
Ni lazima upende
unachokifanya huwezi kufanikiwa kama hupendi unachokifanya, wakati mwingine
pesa huwa hamna na kila kitu huonesha hali ya kukatisha tamaa, lakini kama
unapenda unachokifanya huwezi kukiacha hata kama unapitia wakati mgumu
Uchunguzi unaonyesha watu
ambao hufanya vitu kwa kulazimishwa mara tu wanapopata uhuru wa kuendelea
kufanya au kuacha wengi huamua kuacha.
MARAFIKI ZAO NI WALE WALIOFANIKIWA
Ili uweze kufanikiwa ni
lazima uwe na marafiki waliofanikiwa,
ukiwa na marafiki waliofanikiwa utaishia kupata pesa tu lakini pia utapata
nafasi (opportunity) mbalimbali za kupata pesa ili kuendesha maisha yako
Kama marafiki
waliokuzunguka hawajafanikwa basi utaishia kuwa kama wao , utafanya vitu
wanavyofanya wao, utapiga story kama zao na wala hutajua namna pesa
zinavyotengenezwa, kama wanavyosemaga vitu vinavyofanana hukaa pamoja.
KUWA NA MTAZAMO CHANYA
Asilimia kubwa ya watu
waliofanikiwa wana mtazamo chanya, hupenda kuwachukulia watu katika njia nzuri
ya kujaribu kuwaelewa changamoto zao na kujua namna bora ya kuishi nao, wapo
watu ambao ni wakorofi,wenye hasira na hawakawii kuanzisha ugomvi hivyo lazima
ujua namna nzuri ya kuishi na watu wa namna hiyo.
USIKATE TAMAA
Wapo baadhi ya watu ambao
walijaribu kufanya vitu vikubwa na walikuwa na malengo makubwa lakini walipoona
mambo yameanza kuwa magumu wengi waliamua kutafuta ishu zingine za kufanya,
kukata tamaa ni adui mkubwa wa mafanikia kama unajisikia kukata tamaa tafuta
namna utakavyojifariji ili mradi tu usiache jambo unalolifanya endapo kama una
malengo makubwa kwa hapo baade
FANYA KAZI KWA BIDII
Bidii ya mtu huwa
haipotei fanya kazi zako kwa ustadi wa hali ya juu hapa tunasema (be high
performer), watu wanaofanya kazi kwa ustadi wa hali ya juu ni watu wanaofanya
kazi sana na tunaposema kufanya kazi sana tunamaanisha fanya kazi kila siku
katika masaa yaleyale ambayo umejipangia usiruke baadhi ya siku na kufanya kazi
siku Fulani tu hii itakuchelewesha katika safari yako ya maendeleo,
KITABU CHA SHUGHULI ZA KUFANYA
Mtu yoyote ambae ana
maono fulani ni lazima awe na kijitabu kidogo ambacho ataandika humo mambo
muhimu ambayo anatarajia kuyafanya, kila siku uamkapo asubuhi hakikisha
anaandika vitu vyote ambavyo unataka kuvifanya kwa siku hiyo pamoja na mda utakaozifanya
shughuli hizo hii inaupa ubongo wako nafasi ya kujua ni mawazo ya aina gani
yaje kichwani mwako katika siku hiyo, na wakati mwingine watu hujikuta tu
wakifanya vile vitu ambavyo wameviandika kwanye note buk zao
JIFUNZE KUONGEA MBELE ZA WATU
Ndio! watu ambao
wanauwezo wa kuongea na kutoa hoja huwa wanapata nafasi ya kupewa kipaumbele
katika sehemu yoyote, jifunze namna kumshawishi mtu na kufanya mazungumza yenye
maana mbele za watu, yapo makampuni mengi ambayo yanahitaji watu wanaojua namna
ya kuongea na wateja na kupigia debe bidhaa Fulani, kutetea jambo Fulani kwenye
taasisi au kundi la watu, mtu anapotoa hoja nzuri kwa ujasiri huyo huonekana
ana ufahamu mwingi kupita wengine na ndiye mtu ambaye anaweza akapewa nafasi ya
kufanya kazi Fulani kwa sababu ya uwezo wake wa kuongea
JIAMINI
Kujiamini ni muhimu mno,
mtu ambaye hajiamini huwezi kupanga nae kufanya jambo lolote kubwa kila mtu
mwenye uwezo mpana katika jambo lolote ni mtu anaejiamini na mara nyingi watu
ambao wapo katika safari ya mafanikio hukutana na changamoto nyingi na nyingine
huwa zina vitisho hivyo ni lazima ujiamini ya kwamba unaweza na hakuna jambo
gumu ,kama wengine waliweza wewe una nini mpaka ushindwe?
Hebu jaribu kutafakari na
kujiuliza hivi kwa mfano ungekuwa HUOGOPI CHOCHOTE
HAPA DUNIANI JE UNGECHAGUA KUFANYA NINI? Fikiria kama ungekuwa huogopi
kufa, wala jela, wala polisi, wala kiongozi, wala kazi , wala chochote kile, Je
kwa kutumia ujuzi na hekima uliyonayo SI
UNGESHAFANIKIWA SIKU NYINGI lakini kwa sababu ya uwoga watu wameamua
bora wakae chini watulie na wasifanye chochote kitakacholeta tafrani.
KUWA MTENDAJI
Usipende kuwa mtu wa
maneno matupu kama umepanga jambo basi anza kutenda moja kwa moja, wapo baadhi
ya watu ambao wao kazi yao ni kupanga tu na kutafakari, atasoma vitabu vyote
atasikiliza vitu vitakavyomtia moyo lakini hatochukua hatua yoyote, ni ajabu
kuona watu wanalalamika kwamba mimi ni mnene, mimi sina shepu,mimi sina kazi,
mimi niko hivi lakini mwisho wa siku hafanyi chochote amekaa tu kama mbulula
anasubiri miujiza itoke mbinguni ije imfuate mtu wa namna hiyo hawezi
kufanikiwa hata kidogo ataishia kuwa na matumaini kwamba siku moja na yeye
atafanikiwa lakini ataona miaka inazidi kwenda tu .
NENO LA MWISHO
Mtu aliyefanikiwa na
nguvu za kutenda kazi, hawezi kulalamika, huishi na watu vizuri, ana mtazamo
chanya,huwa ni muongeaji mzuri katika kutetea maslahi Fulani,ni mtu mwenye
maarifa,smart na anajitahidi kuonyesha matokeo mazuri katika kazi yake
anayoifanya
Mtu yoyote aliefanikiwa
ni mtu wa mfano wa kuigwa na mtu huyo anatafutwa na watu wengi ili awasaidie
kuwaingizia pesa kwa sababu ya uwezo na ujasiri wake japo na yeye huwa na
shughuli zake za kufanya.

