NINI KINASABABISHA UGUMU WA MAISHA?
Maisha tunayoishi tunapaswa tuyafurahie na tuishi tukiwa na Amani, lakini kwa sababu moja au
nyingine maisha huonekana kwamba ni magumu, maisha hayapaswi kuwa magumu kama
tutaelewa ni vitu gani vinavyosabisha hali ya maisha ionekanae kuwa ngumu
Hapo chini nitaelezea kwanini maisha ya baadhi ya watu
huonekana kuwa ya taabu na magumu hadi inafika kipindi mtu anakata tamaa ya
kuishi
MAJUKUMU
Majukumu yanapaswa yaendane na uwezo wa kiuchumi katika
maisha ya mtu, mtu anapokuwa ana majukumu mengi kupita uwezo wake wa kiuchumi
hii hufanya mtu kuwa na hofu namna atakavyoweza kuituza familia au watu
waliochini yake kwa mfano unakuta mtu ana watoto wawili halafu kazi hana au
kipato chake ni kidogo mno
Kuna aina mbili za
majukumu
a)Majukumu
ya lazima
haya
ni majukumu ambayo kila mtu huwa nayo wewe kama kijana wa familia Fulani una
jukumu la kusaidia ndugu zako au wadogo zako hapo nyumbani, majukumu kama haya
kila mtu anayo na huwa hayaepukiki
b)Majukumu ya kujitakia
Haya
ni majukumu ya mtu binafsi kwa mfano ameamua kuoa na kuzaa watoto, ameamua
kwenda sehemu za starehe na kutumia hela zake, amepigana na mtu sasa anatakiwa
amlipe fidia au amekopa madeni kwa shida zake inabidi alipe, mara nyingi haya
ndio majukumu yanayofanya maisha kuwa makumu kwa sababu wakati mwingine
majukumu ya kujitakia huwa ni makubwa kuliko uwezo wa mtu
KUKOSA MAARIFA
Ukosefu wa maarifa ni changamoto kubwa sana, maandiko
yanasema si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa, mtu aliyekosa maarifa ya namna
ya kuyaboresha maisha yake hatoweza kuyabadilisha, hivyo ni lazima kujifunza
namna ya kutatua changamoto za kimaisha na kujua ni namna gani utaweza kuongeza
kipato chako, ili uweze kuyahimili majukumu uliyonayo
Udogo wa kipato ni changamoto kubwa ambayo huwakatisha tamaa watu wengi, karibia kila mtu atakwambia hajaridhika na kipato anachopata au kwamba kipato chake hakikidhi mahitaji ya kifamilia , hivyo hupelekea mtu kupata shida na kutafakari atajikwamuaje katika maisha yake, ni vyema mtu kutafuta namna ya kuongeza kipato kwa kufanya biashara ndogondogo za pembeni
Mara nyingi watu wengi ambao wameajiriwa hujiona kwamba wao tayari hawana tena haja ya kuwa na biashara nyingine lakini hii ni mbaya hakuna mtu aliyefanikiwa kwa kutegemea pesa za kuajiriwa ,tafuta mtaji uangalie ni kitu gani unaweza ukafanya kwa ajili ya kuongeza kipato chako
KUSHINDWA KUWEKEZA
PESA ZAKO
Kuwekeza pesa ni jambo la muhimu sana huwezi kufanikiwa
kiuchumi kama huwekezi pesa zako, ndio kipato ni kidogo lakini je katika pesa
unayopata huwa una wekeza kiasi gani kwa ajili ya malengo yako ya baadaye? Utagundua
kwamba watu wengi huwa wahawekezi pesa na hawana pesa yoyote ya ziada kama
likitokea tatizo la ghafla huwa wanaanza kuhaha ni wapi watapata fedha na
mwisho wa siku wengi huishia kukopa madeni hivyo hupelekea hali ya maisha
kuonekana ngumu.
Wapo baadhi ya watu wao kazi yao ni kufikiria vibaya kwenye kila jambo linalotokea, huwezi kufanikiwa kama mtazamo wako ni mbaya lazima ujifunze kuvitazama vitu katika mtazamo chanya kwa mfano limetokea tatizo jiulize tatizo hilo limesababishwa na nini na ni jinsi gani utalitatua na sio kususa, kutukana au kukata tamaa, unaweze ukakemea ukiwa na maneno chanya au kusema dukuduku lako pia kwa maneno chanya.
MAHUSIANO MABAYA NA
WATU
Mahusiano yako na watu huchangia pakubwa katika maendeleo yako ukiona mtu amefanikwa ujue mahusiano yake na watu ni mazuri, hupaswi kutukana watu, au kuwakasirikia watu kwa mambo ya kawaida ongea na watu vizuri kama kuna changamoto tafuteni namna ya kuitatua ili mambo yaishe na mara nyingi vitu ambavyo huja katika maisha ya mtu huletwa kupitia watu waliomzunguka hivyo kama wewe mahusiano yako na watu ni mabaya basi utachelewa sana kufanikiwa maana kitu ambacho ungeweza kukipata kwa mtu Fulani kwa urahisi huwezi kukipata tena kwa sababu ya uhusiano mbovu baina yenu hivyo inabidi usubiri mpaka atakopopatika mtu mwingine mwenye hicho kitu
LAWAMA
Usitafute mtu wa kumlaumu katika maisha yako, ndio maisha
yana changamoto labda haukuweza kusoma kwa sababu wazazi hawakuwa na pesa au
walikuwa hawajali cha muhimu ni kutafuta kujua unatokaje kwenye hali ya maisha
uliyo nayo, unapofanya kazi na watu acha kulalamika na kulaumu watu ovyo,
lazima ujifunze kuwaonyesha watu kwamba wewe ni msaada kwao na kama itatokea
kazi yoyote wanaweza wakakupata bila shida yoyote
Watu wengi wenye lawama hakuna anaeweza kufanya nao kazi
kwa mtu mrefu kwa sababu linapotokea tatizo lolote wao huanza kujitoa na
kutupia lawama watu wengine
Binadamu yoyote anaeishi hapa duniani lazima awe na maono
ya kitu gani anataka kwenye maisha yake, kitendo cha kukosa maono husababisha
mtu kuishi ili mradi tu, mtu kama huyo huwa ana bidii yoyote na haonyeshi
juhudi kwenye kile anachokifanya, mtu anapokosa maono maisha yake huishia kuwa
ya kimaskini kwa sababu hataona haja ya kupambana ili afikie malengo Fulani,
hivyo jitahidi uwe na maono ya nini unatarajia kuwa au nini malengo yako ya
baadaye katika maisha yako.
Mlundikano wa madeni katika maisha ya mtu sio jambo zuri, madeni humfanya mtu kukosa raha katika maisha yake kamwe hautaweza kuwa huru kama una madeni na hasa kama yanazidi uwezo ulionao, lakini pia baadhi ya madeni ambayo watu hukopa huwa yanalipwa kwa riba bado tena kunakuwa na kodi ambazo unapaswa uzilipe mwisho wa siku unajikuta unalipa pesa nyingi ukilinganisha na ulizozikopa
Upukana na madeni, fanya kazi kwa bidii jenga tabia ya
kutunza pesa zako mwenyewe ili zikusaidie kwenye shida ndogondogo za kimaisha ,
NENO LA MWISHO
Epuka kutumia hela zako kwa mkupuo kununua vitu vya
gharama kama simu, luninga na vinginevyo kama kipato chako ni kidogo , wekeza
taratibutaratibu, kisha ndio ununue na sio kuchukua mshahara wote na kuutumia
mara moja, sababu kubwa ya ugumu wa maisha hutokana na udogo wa kipato hivyo ni
muhimu kujifunza namna bora ya kutunza fedha, kuzitumia na namna gani
utajikwamua kiuchumi ili kuweza kufika pale ambapo ulitamani ufike
