jinsi ya kuondoa harafu mbaya kwenye chumba

 

JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA KWENYE CHUMBA

Mara nyingi sana kwenye vyumba tunavyoishi huwa kunakuwa na harufu mbalimbali ambazo husababishwa na vitu tofauti tofauti kwa mfano mlundikano wa nguo chafu au nguo mbichi , viatu ,soksi zilizovaliwa , au ukaribu wa chumba na choo au jalala au uhifadhi wa vitu ambavyo havipaswi kuwepo ndani ya chumba,

    Kuna baadhi ya vitu ambavyo hupaswa kuwekwa stoo and sio chumbani hii hupelekea chumba kuwa na harufu ambayo sio nzuri, zifuatazo ni njia ambazo unaweza kutumia kuondoa harufu mbaya kwenye chumba



Fanya usafi

Fanya usafi na ondoa vitu vyote ambavyo havipaswi kuwepo chumbani ondoa manguo machafu,viatu visafiswe,soksi zifuliwe,shuka za kulalia pia zifuliwe, futa vumbi madirishani hapo utakuwa umekamilisha step ya kwanza ya kuondoa harufu mbaya chumbani

 Tumia air fresher

Air fresher ni nzuri kwa ajili ya kupunguza au kuondoa harufu mbaya chumbani nenda SUPERMARKET au kwenye maduka ambayo fresh air hupatikana, lakini sikushauri utumie perfume kama air fresher kwa sababu perfume huwa na harufu kali kiasi ambacho huweza kusababisha ukawa unapiga chafya tu

 Tumia baking soda

Ndio baking soda huwa ni nzuri katika kuondoa harufu kwa sababu baking soda hufyonza harufu mbaya, hii hutumika pia kwenye kuondoa harufu mbaya za kwenye nguo kwa kuilowekea nguo kwa mda Fulani, kwa hiyo chukua baking soda weka kwenye kikopo au chupa kisha iache wazi basi yenyewe hufyonza harufu yoyote mbaya iliyopo eneo hilo, tembelea  duka lolote la karibu huwa wanauza hizi baking soda

 Tumia white vinegar

White vinegar pia inasifika kwa kufyonza harufu mbaya iwe ni kwenye nguo au chumbani unaposafisha au kudeki chumba unaweza ukaichanganya white vinegar na maji kisha ukayatumia au simply iweke kwenye kopo na uiache wazi kazi yake itakuwa ni kufyonza harufu mbaya kwenye chumba


 Udi

Udi unasifika sana kwa kuwa na harufu nzuri na ndio njia rahisi ya kuondoa harufu mbaya kwenye chumba kwa haraka tembelea madukani ununue udi kisha uwe na tabia ya kuchoma pale unapoona kuna harufu mbaya chumbani

Chemsha viungo na matunda

Unaweza pia ukakatakata malimao au machungwa ukatia kwenye sufuria ukaweka maji pamoja na viungo kama iliki, abdalasini,karafu nk

Kisha ukavichemsha vinapochemka hutoa harufu nzuri  baada ya hapo mimina maji na viungo vyake kwenye kopo kisha liweke mahali likiwa wazi basi ile harufu huendelea kusambaa chumba kizima

 

Post a Comment

Previous Post Next Post