Jinsi ya kumjua/kumtambua nabii wa uongo

  NITAMJUAJE NABII WA UONGO?

Katika zama hizi za sasa watu wanapaswa kuwa makini sana hasa linapokuja kwa watu ambao hudai ya kwamba wametumwa na mungu au wameagizwa na mungu hivyo watu wengi hujikuta wanawaamini watu hawa bila kujiuliza kwa nini watu hawa wanajitahidi kujiaminisha kwao



Kutokana na kutokujua maandiko pamoja na mbinu mbalimbali watu wengi hushindwa kuwatofautisha watu wasemao kweli ya Mungu na watu wasemao uongo, katika ukurasa huu nitakuonesha mbinu mbalimbali zitakazokusaidia kuwajua manabii wa uongo, mitume wa uongo, wachawi pamoja na walimu wa uongo,soma kwa makini ndio utagundua mchezo huu wanaocheza si wa kitoto

UJUMBE MKUU WA MHUBIRI(main message)

Kila mhubiri,Nabii,Mtume,mchungaji n.k huwa na ujumbe mkuu kwa wanadamu(MAIN MESSAGE) , jiulize ujumbe mkuu wa huyo muhubiri ni upi? Toka kuumbwa kwa ulimwengu Mungu hajawahi kumtuma  mtu duniani kuja kufundisha watu jinsi kupata pesa , pamoja na vitu kama nyumba, magari, promotion makazini, kulipwa madeni yao wanayodai,kupata wachumba nk

Vitu hivi huju kwa sababu ya jitihada za mtu na malengo aliyojiwekea kwenye maisha yake,namna anavyoshirikiana na watu,elimu aliyonayo naikadhalika

Watu wote waliotumwa na  Mungu walikuwa na ujumbe mmoja tu kumuonya mwanadamu juu ya jehanamu na kumfundisha namna ya kuishi maisha matakatifu ili kuiepuka jehanamu,

Ni ajabu sana kujua kwamba watu wengi hawajui njia za utakatifu vitu kama kutokuvaa hereni,nywele bandia,mavazi ya stara,kupaka makeup,kuvuta sigara,pombe nk hivi vitu havifundishwi tena eti kwa sababu wanadamu wanapenda kuwa wa kisasa kwa hiyo wahubiri wameamua kuvipuuza na wao

Mtu aliyetumwa na Mungu hawezi kupuuza vitu muhimu hata kama watu wahapendi kuambiwa 

WAHUBIRI WA KIKE

Haijawai tokea na hayupo mhubiri,mchungaji,mtume wa kike kama ukienda sehemu yoyote na ukaona mwanamke anahubiri ujue mwanamke huyo ameenda kinyume na maandiko haijalishi anachohubiri kina umuhimu kiasi gani, Mungu amempa kazi ya kuhubiri mwanaume tu, mwanamke aweza kuwa nabii lakini hapaswi kuhubiri na kuwaonya wanaume masuala ya kuacha dhambi ukumbuke mwanamke ndio aliyesababisha dhambi ikaingia hapa duniani kuna madhara makubwa ya kufundishwa na mwanamke katika kanisa na nitayaanisha kama ifuatavyo

     i.vijana wengi wakiume wanapofundishwa na wanawake kwa mda mrefu hudhoofika na kushindwa kuact kama wanaume majasiri

     ii.wanawake wengi wa kike hujitutumua na kukaza sauti zao kana kwamba wanataka wafanane na wanaume wenye nguvu hiyo siyo mipango ya mungu kwamba mwanamke ashindane na mwanaume

IJARIBU ROHO

Maandiko yanaweka wazi kwamba zijaribuni kila roho, roho zinaweza kujaribiwa kwa kutumia maandiko hapa panahitaji hekima Zaidi mtu ambaye hafahamu maandiko na maana zake inakuwa changamoto kuelewa kama huyo mtumishi anachohubiri ndivyo inavyopaswa au la, ni jukumu la kila mtu kujifunza maandiko na maana zake ili asije mtu akakudanganya kwa kutumia tafsiri za uongo

TAMBUA MAONO

Kuelewa maono na vyanzo vyake ni jambo zuri sana hii inakusaidia kujua chanzo cha ndoto na maono Fulani kwa bahati mbaya sana watu wengi hawaelewi maana za maono na vyanzo vya maono, kila ndoto huwa na chanzo chake na si kila ndoto inahusiana na wewe zingine hazihusiani na wewe kabisa hivyo baada ya kuelewa vyanzo vya maono na vinavyosababisha  ni rahisi kujisababishia ndoto inayohusiana na huyo mtumishi  au mhubiri kwa kutumia product za kwake wakati wa kulala hivyo hupelekea utambuzi wa kiroho kuhusiana na product unazotumia, kama zinanguvu za giza au la,

KUNENA KWA LUGHA

Sual la kunena kwa lugha ni jambo ambalo watu wengi hawajafundishwa wala hawana ujuzi nalo kunena kwa lugha ni jambo la  kimuujiza ( pure miracles) ambapo mtu hunena lugha asiyoijua kabisa wala kuilewa lakini hiyo lugha lazima iwe na maana Fulani akipatikana mtu Fulani aweza kuitafsiri kwamba aliongea amesema kitu gani, uwezo huo wa kutamka maneno hayo huletwa na roho mtakatifu ambaye ni tofauti  na roho yako mwenyewe, cha kushangaza watu wengi hunena kwa lugha kwa kutumia akili zao wenyewe au ubunifu wa kwao, huamua wao mda wa kunena na mda wa kunyamaza, huamua maneno gani watamke na maneno gani wasitamke huyo wala sio roho mtakatifu bali ni wao wenyewe wanajifanya wana roho, hii ipo hata kwa wahubiri na wachungaji huingizia maneno ya lugha wakati wakihubiri waneno ambayo wanajitungia wala hayana maana yoyote.



Post a Comment

Previous Post Next Post