MAMBO YA KUFANYA UNAPOKUWA KWENYE MFUNGO
Soma neno
Neno la mungu Lina nguvu ya
kufanya uponyaji lakini pia unaposoma zaburi huwa pia ni sehemu ya Sala, neno
la mungu litakufariji,litakutia moyo na kukupa tumaini katika Yale magumu
unayopitia
Fanya maombi
Wakati wa mfungo ni lazima
kufanya maombi maana kunakuwa na utulivu katika mlango wa mawazo na hisia pia hivyo mtu huweza kuomba
akiwa na focus ya kutosha
Jihudhurishe mbele
za bwana
Unapokuwa kwenye mfungo usipende
kufunga mpaka mfungo unaisha haujaenda madhabauni kwa bwana nenda kwenye ibada
fanya maombi ukiwa kwenye nyumba ya mungu,
Toa sadaka
Unapokuwa kwenye mfungo toa
sadaka zingine kwa mfano sadaka ya shukrani,sadaka za maombi maalumu,sadaka kwa
ajili ya Toba n.k hii inakuweka kwenye position nzuri ya kiroho katika kujibiwa
maombi yako
Acha kuangalia
TV,kusikiliza miziki ya kidunia,kucheza magemu na kadhalika
Unapokuwa unafunga hupaswi
kufanya Mambo ambayo huwa unayafanya siku zote lazima ustopishe anasa zote za
dunia hii na ufanye Mambo yaliyo safi mbele za Mungu
Ondoa
chuki,lawama,makwazo na Kila Aina ya fitina ndani ya moyo wako
Chuki,kutokusamehe makosa
husababisha mtu kupata maumivu makali ndani ya moyo hivyo kipindi Cha mvungo
unatarajia kupata uponyaji wa moyo,hisia zako na mawazo yako kuwa safi
Usiwaelemee watu
Wasaidie watu wenye shida na hata
wale wanaokusaidia usiwaelemee Kama Kuna task ambazo wanakufanyiaga Basi Sasa
fanya mwenyewe kuwapunguzia mzingo
Pia unaweza kuwapunguzia watu
madeni wale unaowadai ambao unajua Wana kipato Cha chini sana au kuwasamehe kwa wale ambao unajua huyu
uwezo wake wa kipato ni mdogo
